Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kwa masikitiko makubwa, serikali ya Ahmed Tinubu Asiwaju Bola, ambayo kwa sasa iko madarakani nchini Nigeria, pamoja na kujionyesha kuwa ni mtetezi mkubwa wa haki na heshima za kibinadamu, lakini kwa karibu miezi sita sasa imewafunga mamia ya wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria kwa kosa pekee la kushiriki katika maandamano ya Siku ya Quds, bila ya mashitaka yoyote wala mchakato wowote wa kisheria.
Ripoti zinaonesha hali mbaya ya wafungwa hao, kudhoofika na utapiamlo wao, kosa lao ni kushiriki katika mkusanyiko wa amani wa Siku ya Quds ili kuonesha mshikamano na watu wanyonge wa Palestina.
Serikali hii mpya ambayo ilikuja madarakani kwa madai ya haki na demokrasia, wakati wa maandamano hayo ilitoa amri kwa jeshi ili kuwashambulia waandamanaji kwa risasi na virungu, na hatimae kuwaua watu 20, huku wengine wakijeruhiwa na kukamatwa.
Waliokamatwa ni wanaume na wanawake wasio na hatia, na hata miongoni mwao wamo watoto walio chini ya umri wa kisheria. Kwa masikitiko, ukamataji huu si jambo jipya; kwani hata mwaka 2024 baadhi ya Waislamu wa Kishia nchini Nigeria walikamatwa kwa kosa la kushiriki katika ziara ya Atabati Tukufu na safari ya Karbala al-Mu‘alla, na kupelekwa katika gereza la Kafi nchini Nigeria.
Chanzo: Tovuti rasmi ya Harakati ya Kiislamu ya Nigeria
Maoni yako